Agape

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Agape (gir. ἀγάπη, agape) ni neno la lugha ya Kigiriki lenye maana ya "upendo". Ni muhimu hasa katika maandiko ya Agano Jipya na maandiko mengine ya Ukristo, unaojitambulisha kama dini ya upendo.

Kigiriki kina maneno mbalimbali kwa jambo linaloitwa "upendo" katika lugha mbalimbali ambazo zina neno moja tu. Kwa hiyo "agape" inataja maana ya pekee ya "upendo" ambayo ni upendo wa kindugu au upendo wa Mungu. Upande mwingine wa upendo kwa Kigiriki ni "philia" (undugu, pendo lisilo la kingono) na mwingine ni "eros" ambayo ni mapenzi yenye tabia ya kingono.

Agape ni aina ya upendo isiyotafuta faida wala tamaa wala ridhaa.

Katika maandiko ya Kikristo agape inamaanisha:

  • Upendo wa Mungu hasa Kristo kwa binadamu na uumbaji wake
  • Upendo wa binadamu kwa Mungu
  • Upendo wa binadamu kwa mtu mwingine

Chanzo kwa Wakristo ni amri (kiasili ya Agano la Kale) jinsi inavyopatikana kwa mfano katika Luka 10:27:

"Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili yako yote. Na, mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe"

Wakati mwingine namna ya pekee ya kuadhimisha Chakula cha Bwana huitwa "agape".

Christianity Symbol.png Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Agape kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.