Nenda kwa yaliyomo

Robert A. Heinlein

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Robert Anson Heinlein

Robert Anson Heinlein (Julai 7, 1907 - 8 Mei, 1988) alikuwa mwandishi Mmarekani. Aliandika zaidi vitabu vya bunilizi ya kisayansi (SF). Alishinda mara nne tuzo ya Hugo Award, ambayo ni tuzo muhimu zaidi kwa SF.

Kati ya riwaya zake maarufu kuna Starship Troopers ya mwaka 1959, iliyoendelea baadaye kuwa msingi wa filamu na Stranger in a Strange Land ya mwaka 1961, Double Star ya mwaka 1956 na The Moon is a Harsh Mistress ya mwaka 1966. Pamoja na Isaac Asimov na Arthur C. Clarke anatajwa kuwa kati ya waandishi wakuu wa bunilizi ya kisayansi ya Marekani.

Viungo vya Nje

Kuhusu Maisha yake

Kazi zake

Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Robert A. Heinlein kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.