Siku ya wapendanao

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Sehemu ya mfululizo wa makala kuhusu Mapendo
Emblem-favorites.svg

Moyo ni mchoro wa mapokeo ya
Ulaya unaowakilisha mapendo.
Vipengele Msingi
Mapendo kadiri ya sayansi
Mapendo kadiri ya utamaduni
Upendo (fadhila)
Maingiliano ya binadamu
Kihistoria
Mapendo ya kiuchumba
Mapendo ya kidini
Aina za hisia
Mapendo ya kiashiki
Mapendo ya kitaamuli
Mapendo ya kifamilia
Mapendo ya kimahaba
Pia tazama
Mapendo yasiyotuzwa
Ugonjwa wa mahaba
Mapendo cheshi
Uhusiano kati ya watu
Jinsia
Tendo la ndoa
Siku ya wapendanao

Siku ya wapendanao ni sikukuu ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 14 Februari ya kila mwaka (Valentine's Day).

Historia yake imeanzia karne ya 3 huko Roma ambapo alikuwapo padri Valentinus ambaye akaja kuheshimiwa kama mtakatifu hasa tarehe hiyo.

Hadithi zilizosababisha sikukuu kuenea[hariri | hariri chanzo]

Inasemekana kwamba Kaisari wakati huo alikuwa Claudius II: yeye aliona kuwa askari mkakamavu na bora zaidi ni yule asiyeoa wala kuwa na familia (kapera). Hivyo alipiga marufuku ndoa kwa askari.

Valentinus alipinga jambo hili hivyo kuendelea kufungisha ndoa kwa siri. Mfalme Claudius alipopata habari hizi aliamuru Valentinus akamatwe na kuuawa.

Kuna hadithi nyingine ya kuwa akiwa gerezani Valentinus aliandika barua ambayo ilikuwa na salamu za kwanza za Valentine kwa binti aliyekuja kumsalimia gerezani; mwisho wa barua alihitimisha kwa maneno haya: Kutoka kwa Valentinus wako.

Toka hapo Valentine anakumbukwa kama mtetezi wa wapendanao na sikukuu yake kuadhimishwa kote duniani.