Chokoleti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Aina mbalimbali za chokoleti.
Mbegu za kakao ni chanzo cha chokoleti.
Chokoleti hukubali kila umbo: sura ya Yesu kwenye chokoleti.

Chokoleti ni pipi au chakula kitamu kinachotengezwa kwa kutumia kakao, sukari na mafuta. Jina hilo linatumiwa pia kwa kinywaji cha kakao.

Historia ya chokoleti[hariri | hariri chanzo]

Asili yake ni kinywaji cha watu wa Mexiko wa kale waliochemsha unga wa kakao katika maji pamoja na viungo. Wahispania waliikuta kwa Azteki na kuipeleka Ulaya, wakitumia jina la Kiazteki "xocolātl" lenya maana ya "maji machungu".

Katika Ulaya ilitumiwa muda mrefu kama kinywaji, na wakati wa karne ya 19 Wajerumani walianza kutengeneza pipi jinsi inavyojulikana leo.

Chokoleti huyeyuka haraka kwa sentigredi 40-50, hivyo ni rahisi kuifinga kwa maumbo mbalimbali.

Hatua za kutengeneza chokoleti[hariri | hariri chanzo]

  • Chanzo ni mbegu za kakao.
  • Hizo zinakaushwa, kukaangwa na kusagwa. Mbegu zinazosagwa zina kiasi kikubwa cha mafuta ndani yake.
  • Yote yakandamizwa na mafuta ya kakao yanatoka kando.
  • Keki ya kakao inabaki kuwa msingi wa chokoleti.
    • Chokoleti nyeupe hutengenezwa kwa kutumia mafuta ya kakao pekee.
    • Chokoleti ya kawaida huongezwa tena kiasi fulani cha mafuta yake.
    • Chokoleti nyeusinyeusi hubaki bila nyongeza ya mafuta ya kakao.
    • Chokoleti hukorogwa mara nyingi na maziwa na sukari kuwa pipi inayopendwa.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chokoleti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.