Akida

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Akida wa karne ya 2 aliyevaa lorica hamata.

Akida (kutoka neno la Kiarabu) alikuwa mkubwa wa kikosi cha jeshi la zamani, kwa mfano la Dola la Roma.

Katika Biblia ya Kikristo jina hilo linatumika kutafsiri neno la Kilatini "centurio", yaani mkuu wa askari mia.

Maarufu zaidi ni yule ambaye alisimamia utekelezaji wa adhabu ya kifo kwa Yesu akamkiri kuwa kweli Mwana wa Mungu (Mk 15:39), lakini pia yule aliyesifiwa na Yesu Kristo kwa imani yake kubwa (Math 8:5-13: Lk 7:1-10), halafu akida Korneli aliyebatizwa kwa agizo la Mtume Petro bila kudaiwa kwanza atahiriwe (Mdo 10:1-11:30).