Akida Korneli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Petro Akimbatiza Akida Korneli, kadiri ya Francesco Trevisani, 1709.

Akida Korneli (kwa Kigiriki, Κορνήλιος, Kornelios) alikuwa akida wa jeshi la Dola la Roma aliyefanya kazi huko Kaisarea Baharini (Palestina). Huko alivutiwa na dini ya Uyahudi hata akajitolea kujenga sinagogi, pamoja na kusali.

Wongofu wake na wa jamaa zake unasimuliwa mara tatu na Matendo ya Mitume kwa jinsi ulivyotiwa maanani na Luka mwinjili aliyetaka kueleza kwamba desturi ya kubatiza watu wa mataifa bila kudai kwanza watahiriwe ilianzisha na Mtume Petro kwa kuangazwa na Mungu.

Suala hilo lilisumbua sana Kanisa la mwanzo hata baada ya Mtaguso wa Yerusalemu (49 BK) kupitisha desturi hiyo (Mdo 15).

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Saint-stub-icon.jpg Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Akida Korneli kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.