Nenda kwa yaliyomo

Nepal

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Nepali)
नेपाल
Nepāl
Bendera ya Nepal Nembo ya Nepal
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: जननी जन्मभूमिष्च स्वर्गादपि गरीयसी  (Sanskrit)
"Mama na Taifa heri ya Mbinguni"
Wimbo wa taifa: Rastriya Gaan
Lokeshen ya Nepal
Mji mkuu Kathmandu
27°42′ N 85°19′ E
Mji mkubwa nchini Kathmandu
Lugha rasmi Kinepali
Serikali Jahmuri ya shirikisho
Bidhya Devi Bhandari (विद्या देवी भण्डारी)
Pushpa Kamal Dahal
Maungano ya temi za Nepal
{{{established_events}}}
{{{established_dates}}}
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
147,516 km² (ya 93)
2.8
Idadi ya watu
 - Julai 2022 kadirio
 - 2011 sensa
 - Msongamano wa watu
 
30,666,598 (ya 49)
26,494,504
180/km² (ya 62)
Fedha Rupia ya Nepal (NRs.)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
NPT (UTC+5:45)
(haitumiki) (UTC+5:45)
Intaneti TLD .np
Kodi ya simu +977

-


Ramani ya Nepal

Nepal ni nchi ya Asia ya Kusini iliyoko kwenye milima ya Himalaya na inayopakana na Uhindi na China.

Jina rasmi ni jamhuri ya kidemokrasia ya shirikisho la Nepal.

Mlima Everest ambao ni mlima mrefu kuliko yote duniani uko Nepal.

Mji mkuu ni Kathmandu.

Jiografia na hali ya hewa

Nepal ina umbo la mstatili ulioambatanishwa na umbo la pembetatu. Ina urefu wa kilomita takribani 800 na upana wa kilomita 200.

Maeneo ya kijiografia ya Nepal yanayojulikana sana ni Himal, Pahad na Terai: Himal ni eneo lenye milima. Terai ni pahala palipo chini na Pahad ni milima isiyo na theluji.

Kwa kawaida nchi ya Nepal huwa na mvua ya kutosha japo kuna baridi nyingi za kipupwe.

Misitu ya nchi hii imekuwa ikififia kutokana na ukataji holela wa miti.

Historia

Vyombo vya watu waliokuwa wakiishi katika zama za mawe zilipatikana katika bonde la Kathmandu kuonyesha kwamba kumekuwa na watu waliokuwa wakiishi katika eneo hili la Himalaya kwa muda wa zaidi ya miaka elfu kumi na moja. Maandishi makongwe yaonyesha kwamba Nepal ilikuwepo hata miaka 30 kabla ya ujio wa Yesu Kristo.

Viongozi wa kwanza nchini Nepal walikuwa wanaKirati. Historia ya Nepal yaonyesha kwamba kulikuwa na kadri ya himaya 30 za wanaKirati walioongoza nchi hii.

Siasa

Kisiasa Nepal iko katika kipindi cha mageuzi. Hadi mwaka 2006 mfalme alitawala peke yake baada ya kuvunja bunge. Mwaka huo alilazimishwa kurudisha bunge, nalo lilitangaza ya kwamba mfalme hana mamlaka tena likamteua Mkuu wa nchi kwa muda. Tena kwamba bunge jipya litakalochaguliwa mnamo Juni 2007 litaamua juu ya katiba mpya.

Tarehe 28 Mei 2008 wananchi waliamua kumaliza ufalme Nepal ikatangazwa kuwa jamhuri inayofuata demokrasia na kuwa na muundo wa shirikisho.

Katiba mpya ilipitishwa mwaka 2015.

Watu

Wanepali wakicheza ngoma ya asili

Wenyeji wametokana na wahamiaji waliotokea India, Tibet, China na Myanmar.

Hata lugha zinazotumika ni za jamii 4 tofauti. 44.6% wanaongea Kinepali ambacho ndicho lugha rasmi. Hicho ni mojawapo ya lugha za Kihindi-Kiulaya.

Wakazi wengi (81.3%) hufuata dini ya Uhindu. Ubuddha una 9% wa wakazi, ukifuatwa na Uislamu (4.4%), Ukirati (3.1%), Ukristo (1.4%) na dini za jadi (0.4%).

Utalii

Utalii ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Nepal. Nchi hii hupendwa na watalii wanaopenda kuzuru na kuikwea milima yake kama mlima Everest, milima ya Himal na Pahad.

Mengine yanayowapendeza watalii ni kuwatazama ndege wa nchi hii na kupaa juu angani kwa kutumia baluni zilizo na hewa iliyopashwa moto.

Watalii pia hupenda kuzuru nchi hii kwa sababu ya dini ya Kibudha ambayo imejikita mizizi.

Chakula cha Wanepali ni dal bhat. Dal ni mchuzi uliowekwa maharage, nayo bhat ni mchele. Wanepali pia hupenda kula mboga zinazoitwa tarkari zilizowekwa viungo kwa jina chutni.

Picha


Tazama pia

Viungo vya nje

Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nepal kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.