Everest (mlima)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mlima Everest)

Coordinates: 27°59′17″N 86°55′31″E / 27.98806°N 86.92528°E / 27.98806; 86.92528

Mlima Everest
Mlima Everest na theluji

Mlima Everest ni mlima mkubwa kabisa duniani, wenye kimo cha m 8,848 juu ya usawa wa bahari. Ni sehemu ya safu ya milima ya Himalaya.

Kilele chake kipo katika mpaka wa Nepal na China (Tibet).

Watu wa kwanza wa kufika kwenye kilele walikuwa Edmund Hillary wa New Zealand na sherpa Tenzing Norgay wa Nepal tarehe 29 Mei 1953.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Wenyeji upande wa Nepal huuita mlima "Sagarmatha" (सगरमाथा, Mungu mama wa anga) na majirani upande wa Tibet huuita "Qomolangma" ("Mama wa dunia").

Wazungu waliokuwa wa kwanza wa kuchora ramani ya sehemu zile wakauita mwaka 1852 "Mlima XV“. Jina la Everest lilianza kutumiwa na Waingereza tangu mwaka 1865 kwa heshima ya Sir George Everest aliyekuwa mpimaji mkuu wa ramani wa Uingereza kwa sababu alikuwa ameonyesha bidii kubwa katika upimaji wa Uhindi wa Kiingereza.

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Everest (mlima) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.