Tenzing Norgay

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Tenzing Norgay

Tenzing Norgay (*Mei 19149 Mei 1986) alikuwa sherpa kutoka nchi ya Nepal aliyekuwa pamoja na Edmund Hillary mtu wa kwanza wa kukanyaga kilele cha Mlima Everest tar. 29 Mei 1953.

Alikuwa mtoto wa wakulima maskini aliyezaliwa wakati wa kuhiji kwa wazazi wake huko Tibet. Kijana alianza kazi ya kuongoza watalii na wapanda milima jinsi walivyofanya wanaume wengi wa kabila lake.

Akiongozana na misafara kwenye milima ya Himalaya tangu 1935 alijaribu mara kadhaa kupanda mlima Everest bila kufaulu. Mwishowe akiongozana na Edmund Hillary walifika kwenye kilele katika msafara wa Mei 1953.

Kwa miaka mingi watu kutoka Asia na Ulaya walivutana kuhusu swali kama Tenzing au Hillary alikuwa mtu wa kwanza wa kufika kilele. Wote wawili wamekuwa marafiki wakajibu ya kwamba walifika pamoja bila kubagua nani alikuwa mbele hatua chache.

Baadaye mwana na mjukuu wa Tenzing walifika pia kwenye kilele cha Everest.