Msumbiji (kisiwa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kanisa la Mt. Antonio
Daraja la Kisiwa cha Msumbiji linalounganisha kisiwa na bara

Kisiwa cha Msumbiji au kwa lugha ya Kireno "Ilha de Moçambique" ni kisiwa kidogo na pia mji kilichopo 3 km mbele ya mwambao wa Msumbiji ya kaskazini. Urefu ni 3 km na upana kati ya 500 hadi 200 m. Kisiwa ni sehemu ya mkoa wa Nampula. Mji huu ni chanzo cha koloni ya Kireno ya Msumbiji ilikuwa mji mkuu wa nchi kwa karne kadhaa.

Leo hii mji umepanuka kote kisiwani. Kuna wakazi 60,000 wanoishi katika mji mwenye sehemu mbili: mji wa mawe upande wa kaskazini na mji wa makuti upande wa kusini. Kisiwa kilikuwa mji mkuu wa Msumbiji wakati wa ukoloni wa Ureno hadi mwaka 1898 BK.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Habari za kwanza za Kisiwa cha Msubiji zimetokana na Wareno. Alipofika Vasco da Gama mwaka mwaka 1498 BK kisiwa kilikuwa mji wa Waswahili na Waarabu na kituo muhimu cha biashara ya kimataifa katika Bahari Hindi.

Mwaka 1507 Wareno walijenga kituo cha kijeshi. Jengo la kale kisiwani ni kanisa dogo la Nossa Senhora de Baluarte lililojengwa mwaka 1522 BK. Tangu mwaka 1558 hadi 1620 Wareno walijenga boma kubwa la Mtakatifu Sebastiano kwa gharama kubwa. Mawe yote yalichukuliwa kwa meli kutoka Ureno, Goa (Uhindi) na pia pwani la Msumbiji penyewe. Umuhimu wa Msumbiji machoni pa Wareno ulikuwa nafasi ya kituo chenye usalama cha safari nedu kati ya Ureno na Bara Hindi.

Kisiwa kilikua kituo kikuu cha Wareno katika Afrika ya mashariki hasa baada ya kupotea Boma la Yesu huko Mombasa. Waholanzi pia Wafaransa walishambulia kisiwa lakini walishindwa kuteka boma lenyewe.

Mwanzoni Msumbiji ilitawaliwa kama sehemu ya Uhindi ya Kireno kutoka mji mkuu wa Goa. Mwaka 1720 Msumbiji ilikuwa kama jimbo la pekee na kisiwa cha Msumbiji kikawa mji mkuu. Kisiwa kilikuwa bandari muhimu katika biashara ya watumwa kwa visiwa vya Bahari Hindi na pia hadi Brazil ya Kireno.

Mwaka 1898 mji mkuu ulihamishwa kwenda Lourenco Marques (leo Maputo). Kisiwa kilianza kurudi nyuma. Katika miaka ya 1960 daraja lilijengwa kati ya kisiwa na bara.

Idadi ya watu kisiwani imezidi. Walio wengi wanaishi bila maji au choo. Nafasi ya kila mtu ni 27,6 m² pekee.

Urithi wa dunia[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya kuhamishwa kwa mji mkuu kisiwa kilikuwa makao ya Gavana Mkuu wa Msumbiji, wa askofu, wa balozi za nchi kadhaa na wanfanyabiashara kutoka India, Ujerumani, Usiwsi, Ufaransa na Uingereza. Mabaki yao ni majengo ya kihistoria ambayo ni mfano wa pekee wa mji wa kikoloni hasa kwa sababu ujenzi mpya haukutokea baada ya kuondoka kwa makao ya serikali. UNESCO iliandikisha mji wa mawe katika orodha ya Urithi wa Dunia

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]