M'banza-Kongo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mahali pa M’banza Kongo nchini Angola

M'banza-Kongo ni mji wa Angola ya Kaskazini wenye wakazi 25,000 na pia makao makuu ya mkoa wa Zaire ndani ya Angola. Iko karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwenye 6°16′0″S 14°15′0″E.

M'banza-Kongo ilikuwa mji mkuu wa Ufalme wa Kongo ikaitwa kwa karne kadhaa "São Salvador do Congo".

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mji ulikuwepo tayari wakati wa kufika kwa Wareno mnamo mwaka 1498. Ilikuwa mji mkuu wa Manikongo. Hadi leo mti wa Jalankuwo ambako Manikongo aliketi kama Hakimu mkuu umesimama katika eneo la jumba la kifalme la kale. Wakati ule mji uliitwa "Mji wa Kongo" na baadaye "San Salvador wa Kongo" kwa heshima ya Yesu Kristo.

Kuna maghofu ya makanisa mbalimbali ya karne ya 16. Kanisa Kuu lililojengwa 1549 lasemekana ni kanisa kuu la kwanza katika Afrika Kusini ya Sahara na Ethiopia. Lilitembelea na Papa Yohane Paulo II alipozuru Angola 1992.

Ulikua mji mkubwa wakati ya mfalme Afonso I wa Kongo. Taarifa ya kanisa vya miaka ya 1630 yasema kulikuwa na batizo 4,000 hadi 5,000 mjini na katika nchi ya karibu kwa mwaka hivyo wataalamu wamekadria idadi ya wakazi kuwa 100,000.

Mji uliharibiwa wakati vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1665. Wakazi wote walitoka na kuacha maghaofu matupu 1678. Lakini 1709 mfalme Pedro IV of Kongo akarudisha mji mkuu wa milki yake hapo. Umeendelea kukaliwa hadi leo ingawa idadi ya watu ilibadilika mara nyingi.