Kijula
Kijula (au Kidyula) ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Burkina Faso, Cote d'Ivoire na Mali inayozungumzwa na Wajula. Ni lugha ya taifa ya Burkina Faso. Mwaka wa 1990 idadi ya wasemaji wa Kijula nchini Burkina imehesabiwa kuwa watu milioni moja. Pia kuna wasemaji 179,000 nchini Cote d'Ivoire na 50,000 nchini Mali. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kijula iko katika kundi la Kimande.
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
- lugha ya Kijula kwenye Multitree
- makala za OLAC kuhusu Kijula
- lugha ya Kijula katika Glottolog
- http://www.ethnologue.com/language/dyu
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kijula kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |