Wabobo
Wabobo ni watu wa kabila la kundi la Wamande wanaoishi hasa nchini Burkina Faso, na wengine wanaishi kaskazini mwa nchi ya Mali. Jina lao limeingia katika lile la mji wa pili kwa ukubwa nchini Burkina Faso, Bobo-Dioulasso.
Usuli
[hariri | hariri chanzo]Katika fasihi nyingi za sanaa ya Kiafrika, kundi linaloishi katika eneo la Bobo-Dioulasso linaitwa Bobo-Fing, maana yake halisi ni "Bobo mweusi". Watu hao wanajiita Wabobo na wanazungumza lugha ya Kibobo, ikiwa kama sehemu ya lugha za Kimande. Wabambara pia wanaita kundi lingine la kikabila "Wabobo", yaani Bobo-Oule/Wule, ambao kwa usahihi wanaitwa Wabwa. Wakati Wabwa (Bobo-Oule) ni watu wa Gur, wanaozungumza lugha za Gur (lugha za Wabwa), Wabobo wa kweli (Bobo Madare, Bobo Fing) ni watu wa Mande.
Takwimu za kijiografia
[hariri | hariri chanzo]Wabobo wako karibu 110,000, wengi wao wakiwa nchini Burkina Faso. Jamii kubwa ya Wabobo huko kusini ni Bobo-Dioulasso, mji wa pili kwa ukubwa nchini Burkina Faso na mji mkuu wa zamani wa Volta ya Juu, koloni la Ufaransa. Kaskazini zaidi kuna miji mikubwa, ikiwemo Kigezo:Interlanguage link multi na Kouka, na Boura kaskazini kabisa mwa Mali.
Wabobo ni wazawa wa mkusanyiko wa zamani ambao waliungana karibu na idadi kadhaa ya koo za awali, hakuna hata moja ambayo ilihifadhi masimulizi ya mdomo kwenye eneo hilo. Lugha na utamaduni wa Wabobo vinahusiana zaidi na wale wa majirani zao wa Mandé kaskazini na magharibi, yaani watu wa Wabamana (pamoja na Minianka, pia inajulikana kama Mamara Senoufo, na watu wa Gur) kuliko majirani zao wa Voltaic Wagurunsi na Wamossi, lakini wanapaswa kufikiriwa kama upanuzi wa kusini wa watu wa Mandé ambao wanaishi katika eneo ambalo sasa ni Burkina Faso, badala ya kundi la Mandé lililoingia hivi karibuni katika mkoa huo. Ingawa zaidi ya 41% ya koo za Wabobo wanadai asili ya kigeni, pia wanasema kuwa wao ni wakazi wa asili katika eneo husika.
Uchumi
[hariri | hariri chanzo]Kilimo ni miongoni mwa vitu muhimu sana kwa Wabobo. Shughuli za kilimo siyo tu njia ya kujikimu miongoni mwa Wabobo, ni sehemu muhimu ya maisha yao ya kila siku. Mazao makuu ya chakula ni sorghum nyekundu, mtama wa lulu, [viazi vikuu]], na mahindi. Pia wanalima pamba, ambayo inauzwa kwa viwanda vya nguo huko Koudougou. Uwekaji wa utawala wa kikoloni na ujenzi wa viwanda hivi ulisababisha kuvunjika kwa mifumo ya kazi ya pamoja, ambayo ilikuwa ikiwafunga wanachama wa jamii ya Wabobo pamoja.
Mfumo wa kisiasa
[hariri | hariri chanzo]Wabobo ni kundi la watu ambao hawana utawala wa kati. Wazo la kuweka mamlaka ya kisiasa mikononi mwa mtu binafsi ni geni kwa Wabobo. Kila kijiji kimepangwa kulingana na uhusiano kati ya koo za kiumeni. Koo inawaunganisha wote waliotokana na babu mmoja wa kawaida, anayeitwa wakoma, neno ambalo shina lake, wa-, ni ufupisho wa neno la Wabobo la nyumba wasa. Koo ya Wabobo inajumuisha watu wanaoishi katika nyumba moja. Kiongozi wa koo anaitwa wakoma au baba wa koo. Anaweza pia kuitwa sapro, ambalo ni neno la mababu.
Dini
[hariri | hariri chanzo]Mungu Muumba anaitwa Wuro. Hawezi kuelezeka na haonyeshwi na sanamu. Hekaya za Wabobo kuhusu uumbaji wa ulimwengu na Wuro na mpangilio wa viumbe wake. Yeye ndiye anayehusika na mpangilio wa vitu vyote duniani kuwa jozi zinazopingana: mwanadamu/roho, mwanamume/mwanamke, kijiji/msituni, utamaduni/asili na kadhalika. Uwiano kati ya nguvu kama zilivyoumbwa na Wuro ni dhaifu, na ni rahisi kwa mwanadamu kuharibu uwiano huo. Kilimo, kwa mfano, kinaweza kuvuruga uwiano dhaifu kati ya utamaduni/asili na kijiji/msituni wakati mazao yanapokusanywa msituni na kuletwa kijijini. Kwa watu wa Wabobo kuna vipindi viwili muhimu. Wakati wa Wuro, wakati ulimwengu uliumbwa na wakati wa kihistoria, wakati Wuro alimpa mwanadamu mwana wake Dwo.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- Christopher Roy: Art of the Upper Volta Rivers. Traduction et adaptation en francais F.Chaffin. Alain et Françoise Chaffin, Meudon, 1987
- Guy Le Moal : Les Wabobo. Nature et fonction des masques. Musée royale de l'Afrique centrale, Tervuren, 1999.
Makala hii ni sehemu ya warsha ya kuhariri Wikipedia huko MUM. Unaweza kusaidia kuihariri na kuongeza habari. |