Kijeri
Kijeri ni jina badala linalotumika kutajia lugha mbili za Kimandé zinazozungumzwa kaskazini-magharibi mwa Ivory Coast na kusini-magharibi mwa Burkina Faso.
Lugha hizo mbili zilifikiriwa hadi hivi karibuni kuwa lahaja za lugha moja, lakini sasa zinajulikana kuwa ni lugha mbili tofauti kabisa. Lugha ya Burkina ni Kijalkunan (Kiblé, Kidyala, Kidyalanu, Kijalanu), na lugha ya Ivory Coast ni Kijeri-Kuo (Kicelle, Kijeli Kuo).[1]
Kijeri-Kuo inazungumzwa na watu ambao kwa jadi walikuwa wachache wa tabaka katika eneo ambalo kwa kiasi kikubwa linazungumzwa lugha za Kisenufo. Lugha hii inadhaniwa kuwa inatishiwa kutoweka, na 90% ya watu wa kabila la Jeri wamehamia lugha zinazotawala katika eneo hilo. Watu wanaozungumza Kijalkunan wa kijiji cha Blédougou sio watu wa tabaka, ingawa vijiji jirani vya makabila mengine vina sehemu nzima zinazokaliwa na tabaka za wafua vyuma na watengeneza ngozi. Lugha ya Kijalkuna inabadilishwa na Jula (Dioula), lakini haiko hatarini kutoweka mara moja.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]
Makala hii ni sehemu ya warsha ya kuhariri Wikipedia huko MUM. Unaweza kusaidia kuihariri na kuongeza habari. |
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kijeri kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |