Wabambara
Mandhari
Wabambara ni kabila la Afrika ya Magharibi. Wanatumia lugha ya Kibambara, moja ya lugha za Kimande.
Wengi wao huishi katika nchi ya Mali ambako lugha yao ni lugha ya taifa. Wako pia katika Guinea, Senegal, Burkina Faso, Niger, Ivory Coast, Mauritania na Gambia.
Idadi yao hukadiriwa kuwa milioni 6-7 nchini Mali.[1]
Asili ya Wababambara ni kuwa tawi la Wamandinka. Katika karne ya 13 Wabambara walianzisha Milki ya Mali. Leo hii wengi wao hufuata dini ya Uislamu.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ CIA World Fact Book, inakadiria theluthi moja kati ya wakazi milioni 20 kuwa Wababambara (iliangaliwa Julai 2021).