Ulaya ya Kati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ulaya ya Kati

Ulaya ya Kati ni kanda ya bara la Ulaya iliyopo baina ya Ulaya ya Mashariki na Ulaya ya Magharibi.

Katika mpangilio wa Umoja wa Mataifa unaofuata kawaida ya miaka ya Vita baridi hakuna Ulaya ya Kati kwa sababu wakati ule kitovu cha Ulaya kiligawiwa kisiasa kati ya mashariki (Umoja wa Kisovyeti) na magharibi (NATO). Hata hivyo kiutamaduni watu wa sehemu zile hawajisikii kama watu wa Ulaya ya Magharibi wala Mashariki.

Kwa kawaida nchi zifuatazo huhesabiwa kama sehemu za Ulaya ya Kati:

Kihistoria nchi hizi zote ziliwahi kuwa sehemu za madola makubwa ya Dola la Ujerumani na Austria-Hungaria.

Kuna majadiliano kuhusu mipaka ya kanda hili yasiyokwisha bado, kwa mfano swali la nchi za Kibalti kama Latvia.