Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Italia

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Italia peninsula - rasi

[hariri chanzo]

Sina uhakika kama neno "peninsula" limeshapokelewa katika Kiswahili. Naikumbuka kwa redio China (huduma ya Kiswahili). Lakini menginevyo nimekuta mara kwa mara "rasi" linalotaja maeneo makubwa (rasi ya Italia, rasi ya Iberia, rasi ya Korea) au sehemu ndogo kama vile Rasi ya Tumaini Jema. Lakini sipati nafasi ya kusoma ya kusoma magazeti hapa. Naomba tu ukibadilisha neno (jinsi ulivyofanya katika makala Vatikani) ni vema kuangalia kama tuanyo tayari matumizi hapa kwenye wikipedia. Kwa sasa nimetumia kwa kawaida neno "rasi" katika makala mbalimbali za kijiografia. Ukiona kuna msingi wa kutumia "peninsula" naomba utaje tushauriane. Kama ni kweli neno jipya "peninsula" basi tutumie kote? --Kipala (majadiliano) 11:15, 8 Februari 2009 (UTC)[jibu]