Nenda kwa yaliyomo

Pato la taifa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka JPT)
Nchi kulingana na pato lake la taifa mnamo 2014.

Pato la taifa au jumla ya pato la taifa (kifupi: JPT) ni kipimo cha thamani ya sokoni ya bidhaa na huduma zote zinazozalishwa ndani ya nchi katika muda fulani.[1]

JPT hutumiwa kwa kawaida na serikali ya nchi ili kupima afya ya uchumi wake. Kipimo hicho mara nyingi hurekebishwa kabla ya kufikiriwa kuwa kiashiria cha kuaminika.[2]

Pato halisi la taifa

[hariri | hariri chanzo]

Pato kamili, yaani pato lisilorekebishwa, halihesabu gharama za maisha zinazotofautiana nchi kwa nchi. Kwa hiyo, wachumi mara nyingi hutoa taarifa ya pato halisi la taifa. Thamani hiyo ndiyo inayohesabu tofauti za uwezo wa ununuzi unaosababishwa na gharama za maisha. Pato halisi la taifa hupatwa kwa kukokotoa kima cha uwezo sawa wa ununuzi.[3]

  1. Duigpan, Brian (2017-02-28). "gross domestic product". Encyclopedia Britannica (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-02-25. Iliwekwa mnamo 2023-02-23.
  2. "What Is GDP and Why Is It So Important to Economists and Investors?" (kwa Kiingereza). Investopedia. Iliwekwa mnamo 2023-05-05.
  3. Hall, Mary. "What Is Purchasing Power Parity (PPP)?". Investopedia (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Novemba 2016. Iliwekwa mnamo 23 Februari 2019.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pato la taifa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.