Mto Tiber

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Tiber)
Jump to navigation Jump to search
Njia ya Mto Tiber katika ramani ya Italia ya Kati.
Mto Tiber ndani ya mji wa Roma (kuba kubwa ni la Basilika la Mt. Petro)

Tiber (kwa Kiitalia: Tevere, kutoka Kilatini Tiberis) ni mto nchini Italia.

Chanzo chake kipo kwenye milima ya Apenini karibu na mlima Monte Fumaiolo katika mkoa wa Emilia-Romagna, halafu mto unapita kilomita 405 katika mikoa ya Toscana, Umbria na Lazio ikipita katika mji wa Roma hadi kufikia mdomo wake kwenye Bahari ya Mediteranea karibu na bandari ya kale ya Ostia Antica.