Mto Tiber

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Njia ya Mto Tiber katika ramani ya Italia ya Kati.
Mto Tiber ndani ya mji wa Roma, kwenye "Daraja la Mt. Malaika" (Ponte St Angelo); kuba kubwa nyuma ni la Basilika la Mt. Petro).
Alama ya mafuriko ya Roma, 1598, iliyowekwa kwenye nguzo ya Hospitali ya Santo Spirito karibu na Basilika la San Pietro.

Tiber (kwa Kiitalia: Tevere, kutoka Kilatini Tiberis) ni mto nchini Italia.

Chanzo chake kipo kwenye milima ya Apenini karibu na mlima Monte Fumaiolo katika mkoa wa Emilia-Romagna, halafu mto unapita kilomita 405 katika mikoa ya Toscana, Umbria na Lazio ikipita katika mji wa Roma hadi kufikia mdomo wake kwenye Bahari ya Mediteranea karibu na bandari ya kale ya Ostia Antica.

Mto ulikuwa muhimu katika historia ya mji wa Roma maana mji huo ulianzisha sehemu ambako iliwezekana kuvuka mto Tiber kwa miguu.

Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Tiber kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.