Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ni shirika la kimataifa ambalo ofisi yake kuu iko Geneva, Uswisi. Kamati ilianzishwa na Henri Dunant chini ya jina Kamati ya Watano tarehe 9 Februari 1863. Shabaha zake hasa ni kuwasaidia na kuwalinda watu wakati wa vita. Kamati imezawadiwa Tuzo ya Nobel ya Amani mara tatu: miaka ya 1917, 1944, na 1963.

Siku hizi, kamati ni mwanachama wa Shirika za msalaba mwekundu na hilali nyekundu.