Shirika za msalaba mwekundu na hilali nyekundu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera za Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu

Shirika za msalaba mwekundu na hilali nyekundu (kifupi: Msalaba Mwekundu) ni harakati ya kimataifa ya kulinda maisha ya kibinadamu hasa wakati wa vita.

Taasisi zake ni

Shirika hizi zinalenga kulinda maisha ya kibinadamu na kusaidia watu wenye matatizo ya kiafya kote duniani bila kujali utaifa, rangi au dini.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Msalaba Mwekundu ulianzishwa na mfanyabiashara Mswisi Henry Dunant baada ya mapigano ya Solferino wakati wa vita ya Austria dhidi ya Italia na Ufaransa 1859. Siku ile wanajeshi 6000 walikufa na 25,000 walijeruhiwa. Dunant alishangaa na kusikitika mateso ya wanajeshi walioachwa mara nyingi mahali pa mapigano akaacha biashara zake kwa siku kadhaa akawasaidia wajeruhiwa. Baadaye alianzisha kempeni ya kuunda na kukubali shirika litakalotunza wajeruhiwa wakati wa vita lisilosimama upande wote na litakalokubaliwa na nchi zote.

Henri Dunant mnamo 1860

1863 aliunda Kamati ya Kimataifa ya shirika za kutunza wajeruhi na kufanya mkutano wa kwanza wa kimataifa. Watu binafsi lakini pia wawakilishi wa serikali kadhaa zilihudhuria. Kamati hili limekuwa chanzo cha Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu ya Geneva ya leo hii.

Kwenye mkutano uliofuata tar. 22 Agosti 1864, nchi 12 zilikubali Mapatano ya Geneva ya kwanza kuhusu usaidizi kwa wanajeshi wanaojeruhiwa wakati wa vita. Makubaliano yalihusu ya kwamba wajeruhiwa hawatashiriki tena katika mapigano, hawatashambuliwa au kuuawa tena, ya kwamba wasaidizi watavaa alama ya msalaba mwekundu na hawatashambuliwa vilevile. Shirika za kitaifa za msalaba mwekundu zitakubaliwa kama serikali ya nchi ilitia sahihi kwenye mapatano ya Geneva.

Mapatano ya Geneva yaliendelezwa katika miaka iliyofuata yakaingiza pia mabaharia na watu raia wasio wanajeshi na haki zao.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]