Uroho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa Evelyn De Morgan kuhusu Ibada ya Mamona 1909.
Vilema vikuu

Uroho ni hamu isiyoratibiwa ya kujipatia mali kuliko mtu anavyohitaji, hata kuwakosesha wengine.

Ni chanzo cha maovu mengi katika maisha ya jamii, kama vile unyonyaji, wizi, vita n.k.

Kwa sababu hiyo maadili ya Kanisa yanauhesabu kati ya vilema vikuu ambavyo vinasababisha dhambi nyingine.

Tena, kadiri ya mtume Paulo, uroho unachangia dhambi zote.