Kitabu cha Tobiti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kitabu cha Tobiti ni kimojawapo kati ya vitabu vya deuterokanoni vya Biblia ya Kikristo.

Nakala zilizopatikana katika mapango ya jumuia ya Waeseni huko Qumran zinaonyesha kuwa kitabu hicho kiliandikwa kwanza kwa Kiaramu miaka 200 KK hivi na kutafsiriwa mapema kwa Kigiriki katika Septuaginta.

Inaonekana kuwa tafsiri ya Kilatini maarufu kwa jina la Vulgata iliyofanywa na Jeromu inategemea andiko asili.

Kitabu hicho kilikubaliwa kama sehemu ya Biblia katika mtaguso wa Cartago wa mwaka 397, halafu tena na Mtaguso wa Trento (1546).

Lakini hakikubaliwi na Wayahudi katika Tanakh, wala na Waprotestanti wengi.

Hadithi hiyo inahusu familia ya kabila la Naftali la taifa la Israeli katika karne ya 7 K.K., baada ya uhamisho uliosababishwa na Waashuru.

Lengo lake kuu ni kufundisha maadili bora ya Wayahudi

Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.


Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDK YudithiDK Esta Wamakabayo IDK Wamakabayo IIDK Yobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DK SiraDK Wimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDK Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.