Kitabu cha Wamakabayo II

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Judea chini ya Yuda Makabayo.

Kitabu cha pili cha Wamakabayo ni kimojawapo katika ya vitabu vya deuterokanoni vya Agano la Kale katika Biblia ya Kanisa Katoliki na ya Waortodoksi wengi.

Sawa na Kitabu cha Wamakabayo I kinasimulia upiganaji uhuru wa Wayahudi wakiongozwa na familia ya Wamakabayo katika karne ya 2 KK, lakini hakikuandikwa na mtu yuleyule, ingawa jina lake halijulikani.

Anadhaniwa kuwa Myahudi msomi wa Aleksandria (Misri) au aliyeathiriwa na shule ya uandishi ya Misri.

Ingawa aliandikwa kwa ufasaha katika lugha ya Kigiriki, anaonekana ameshikilia kabisa Torati ya Uyahudi.

Kitabu kinaonekana kimeandikwa mwishoni mwa karne ya 2 KK kwa kufupisha vitabu vitano vya Yasoni wa Kirene (2Mak 2:19-32).

Kinasimulia kwa namna nyingine habari za awali za Kitabu cha kwanza cha Wamakabayo (176 KK - 160 KK); hivyo si mwendelezo wake, bali kinakikamilisha na kuzidisha mtazamo wake wa imani hasa upande wa Hekalu la Yerusalemu.

Kitabu hicho ni muhimu katika maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa Israeli, kwa kuwa kinafundisha uumbaji kutoka utovu wa vyote, ufufuko wa wafu, maombezi kwa ajili ya marehemu, uwepo wa malaika n.k.

Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki

Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Wamakabayo II kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.