Kitabu cha Kwanza cha Wafalme

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wafalme I)
Jump to navigation Jump to search

Kitabu cha Kwanza cha Wafalme ni sehemu ya Tanakh (Biblia ya Kiebrania na ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo. Hugawiwa katika sura 22.

Historia ya kitabu[hariri | hariri chanzo]

Zamani kilikuwa kitabu kimoja pamoja na Wafalme II lakini katika Septuaginta kitabu kiligawiwa pande mbili. Wataalamu huamini hii ilitokea kutokana na urefu wa kitabu si kwa sababu ya yaliyomo au ya mpangilio wake.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Yaliyomo[hariri | hariri chanzo]

Kinasimulia hasa habari za wafalme wa Israeli ya Kale. Chanzo ni habari za mfalme mzee Daudi na za Solomoni aliyemfuata. Hapa kuna pia maelezo kuhusu ujenzi wa hekalu la Yerusalemu.

Kinachofuata ni habari za ugawaji wa milki kuwa madola mawili yaani:

Habari za nabii Eliya na nabii Elisha pia zinapatikana humo.

Kati ya masimulizi mashuhuri sana ya kitabu hiki ni hukumu ya Suleimani (Wafalme I 3, 16-27).

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDK YudithiDK Esta Wamakabayo IDK Wamakabayo IIDK Yobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DK SiraDK Wimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDK Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

[[Picha:Picha:Mfano.jpg]]