Ahabu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfalme Ahabu katika Promptuarii Iconum Insigniorum.

Ahabu (kwa Kiebrania: אַחְאָב, Aẖ'av, ʼAḥʼāḇ), mwana wa Omri, alikuwa mfalme wa saba katika ufalme wa Israeli. William F. Albright alikadiria utawala wake kuwa miaka 869850 KK, E. R. Thiele miaka 874853 KK[1] na Michael D. Coogan miaka 871852 KK.[2].

Vitabu vya Wafalme vinamchora kama mwovu sana, kwa kufuata mke wake Yezebeli, kumuua Naboti na kuelekeza taifa la Israeli kuabudu miungu mingi, hasa Baali.

Lakini Nabii Elia kwa karama yake ya kutokea na kutoweka hakuweza kuuawa kama manabii wenzake wengi, akafaulu kuokoa imani katika Mungu pekee, YHWH.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Edwin Thiele, The Mysterious Numbers of the Hebrew Kings, (1st ed.; New York: Macmillan, 1951; 2d ed.; Grand Rapids: Eerdmans, 1965; 3rd ed.; Grand Rapids: Zondervan/Kregel, 1983). ISBN 0-8254-3825-X, 9780825438257.
  2. Michael D. Coogan, A Brief Introduction to the Old Testament, (Oxford: Oxford University Press, 2009) 237.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ahabu kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.