Rehoboamu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ufalme wa Muungano ulivyosambaratika, huku Yeroboamu I akijitwalia Israeli Kaskazini (kijani).

Rehoboam (kwa Kiebrania: רְחַבְעָם‬, Rəẖavʻam au Reḥaḇʻām; kwa Kigiriki: Ροβοαμ, Rovoam; kwa Kilatini: Roboam; 970 KK-910 KK hivi) alikuwa mfalme wa nne wa Israeli.

Habari zake zinapatikana katika Biblia (Kitabu cha Kwanza cha Wafalme na kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati).

Alikuwa mtoto na mrithi wa Solomoni[1], lakini alisababisha uasi wa makabila ya kaskazini yakiongozwa na Yeroboamu I, akajikuta amebaki na yale ya kusini tu.

Mama wa Rehoboam alikuwa si Mwisraeli, bali Mwamoni. Mwenyewe alioa wake 18 na masuria 60 na kupata watoto 88: 28 wa kiume na 60 wa kike.

Rehoboamu alitawala miaka 17 akarithiwa na mwanae Abijah.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Before the death of Solomon the apparently unified kingdom of David began to disintegrate. With Damascus independent and a powerful man of Ephraim, the most prominent of the Ten Tribes, awaiting his opportunity, the future of Solomon's kingdom became dubious". Rehoboam". Jewish Encyclopedia. 1906.
Saint-stub-icon.jpg Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rehoboamu kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.