Nabii Shemaya
Nabii Shemaya (kwa Kiebrania שְׁמַעְיָה, Šəmaʿyā, maana yake: "YHWH amesikia"; alikuwa nabii nchini Israeli katika karne ya 10 KK.
Chanzo kikuu cha historia yake ni Kitabu cha Kwanza cha Wafalme (12:22-24) pamoja na Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati (11:2-4; 12:5-7).
Kadiri ya vitabu hivyo, alimzuia mfalme Rehoboamu asipigane vita na Yeroboamu I ili kujirudishia mamlaka juu ya makabila ya kaskazini yaliyoasi[1].
Pia alimtabiria Rehoboamu adhabu ya Mungu kumpitia farao Shishak wa Misri kwa makosa yake.
Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 8 Januari.
Mengineyo
[hariri | hariri chanzo]Katika Biblia ya Kiebrania kuna watu wengine kumi na saba wenye jina hilohilo, tena inataja Kitabu cha nabii Shemaya kama chanzo cha habari kadhaa, lakini kitabu hicho kimepotea hata leo.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Pulpit Commentary on 1 Kings 12, accessed 17 October 2017
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nabii Shemaya kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |