Kitabu cha Hekima

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Kitabu cha Hekima au Hekima ya Solomoni ni cha mwisho kuandikwa (miaka 50 hivi K.K.) katika ya vitabu vya deuterokanoni vya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Hupangwa kati ya vitabu vya hekima, kichwa kinavyodokezwa.

Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mwandishi[hariri | hariri chanzo]

Ingawa mwandishi anajidai kuwa mfalme Solomoni ili kutia maanani ujumbe wake, wataalamu wanasema lugha fasaha na mawazo vinaonyesha wazi asili yake katika mazingira ya Kigiriki ya Aleksandria (Misri).

Alikuwa Myahudi msomi katika dini, falsafa na maadili.

Mafundisho[hariri | hariri chanzo]

Kati ya michango yake upande wa teolojia kuna fundisho la kutokufa kwa roho, lakini pia utabiri juu ya mateso ya Yesu na umilele wa Hekima ya Mungu.

Sala ya kujiombea hekima (Hek 9:1-6)[hariri | hariri chanzo]

"Ee Mungu wa baba zetu, Bwana, mwenye kuihifadhi rehema yako, umevifanya vitu vyote kwa neno lako; na kwa Hekima yako ukamwumba mwanadamu, ili avitawale viumbe vilivyoumbwa nawe, na kumiliki ulimwengu katika utakatifu na kwa haki, na kutoa hukumu kwa unyofu wa moyo. Nakusihi unipe Hekima, ambayo huketi karibu nawe katika kiti chako cha enzi, wala usinikatae mimi miongoni mwa watumishi wako; mimi niliye mtumwa wako, na mwana wa mjakazi wako, mtu dhaifu asiye na siku nyingi, wala sina nguvu ya kufahamu hukumu na sheria. Kwa maana mtu ajapokuwa ni mkamilifu miongoni mwa wanadamu, pasipo Hekima itokayo kwako atahesabiwa kuwa si kitu".

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDK YudithiDK Esta Wamakabayo IDK Wamakabayo IIDK Yobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DK SiraDK Wimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDK Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.