Kitabu cha Yuditi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kitabu cha Yudith)
Jump to navigation Jump to search

Kitabu cha Yudith ni kimojawapo kati ya vitabu vya deuterokanoni vya Biblia ya Kikristo.

Kimo katika Septuaginta na katika Agano la Kale la Kanisa Katoliki, la Waorthodoksi wengi na la baadhi ya Waprotestanti, lakini si katika Tanakh ya Uyahudi wala katika Biblia ya Waprotestanti.

Habari iliyomo[hariri | hariri chanzo]

Hadithi hiyo, iliyoandikwa katika karne ya 1 K.K. inahusu wakati wa mfalme Nebukadreza II, na vita vyake dhidi ya Israeli (karne ya 6 K.K.).

Kinyume cha matarajio, Yudith, ambaye jina lake linamaanisha mwanamke wa kabila la Yuda, aliweza kupata ushindi kwa imani na ushujaa wake.

Habari hiyo ya ajabu ilipata mwangwi kwa wingi katika sanaa mbalimbali.

Ufafanuzi[hariri | hariri chanzo]

Wengi wanaona katika Yudith kielelezo cha Bikira Maria katika mapambano dhidi ya shetani, hasa kutokana na maneno yafuatayo: "Umebarikiwa, binti yangu, usoni pa Mungu Aliye Juu, kuliko wanawake wote duniani. Na ahimidiwe Bwana Mungu, Muumba mbingu na nchi, aliyekuongoza hata ukampiga kichwa mkuu wa adui zetu" (Yudith 13:18).

Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.


Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDK YudithiDK Esta Wamakabayo IDK Wamakabayo IIDK Yobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DK SiraDK Wimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDK Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.