Nenda kwa yaliyomo

Kabila la Yuda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kabila la Yuda ni mojawapo kati ya makabila ya Israeli ambayo kwa jumla ni 12, kutokana na watoto wa kiume 12 wa Yakobo Israeli.

Kabila hilo kubwa la kusini lilishika nafasi muhimu katika historia ya taifa na kushindana na makabila ya kaskazini hata ufalme uligawanyika pande mbili: Israeli na Yuda.

Baada ya ufalme wa kaskazini kukoma mwaka 722 KK, ule wa kusini ulibaki peke yake hadi ulipokomeshwa mwaka 586 KK (maangamizi ya Yerusalemu na mwanzo wa uhamisho wa Babeli).

Hata hivyo, mwaka 538 KK watu wa kabila hilo (pamoja na wa kabila la Lawi na wachache wa kabila la Benyamini) walianza kurudi Yersusalemu wakaitwa Wayahudi.

Mtu maarufu zaidi wa kabila hilo ni Yesu aliyekuwa mwana wa Bikira Maria, lakini alijulikana kama mtoto wa Yosefu wa ukoo wa mfalme Daudi na kwa hiyo wa kabila la Yuda. Ndiyo sababu aliitwa Mwana wa Daudi na Simba wa Yuda.

Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kabila la Yuda kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.