Nenda kwa yaliyomo

Lutu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kuondoka kwa Abrahamu na Lut, nakshi (432-440) huko Roma, katika Basilika la Santa Maria Maggiore.

Lutu (kwa Kiebrania לוט - lōṭ; kwa Kiarabu لوط - lūṭ) alikuwa mtoto wa Haran, mdogo wa Abrahamu kadiri ya Biblia na Kurani, ambaye alimfuata kutoka Mesopotamia hadi Kanaani.

Katika Biblia habari zake zinapatikana hasa katika kitabu cha Mwanzo, ambapo sura ya 19 inatuchorea uovu wa watu ambao huko Sodoma ulizidi hata kumdai Mungu alipe kisasi.

Lakini kati yao mwadilifu Lutu akaokolewa, isipokuwa mke wake akaja kuadhibiwa kwa sababu aliangalia nyuma, kinyume cha agizo la Bwana (Lk 17:28-33).

Lutu alikuwa na sifa ya ukarimu maana aliwakaribisha wageni waliokuwa malaika ingawa yeye hakujua; kwa hiyo tusiache kufuata mfano wake huo.

Lutu ndiye baba wa makabila ya Wamoabu na Waamoni, waliokaa upande wa mashariki wa mto Yordani (leo nchini Yordani).

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lutu kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.