Nenda kwa yaliyomo

Mtende (mti)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtende
(Phoenix dactylifera)
Mitende ya kawaida huku Maroko
Mitende ya kawaida huku Maroko
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Arecales (Mimea kama mpopoo)
Familia: Arecaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mpopoo)
Jenasi: Phoenix
Spishi: nyingi

Mitende ni miti mikubwa ya jenasi Phoenix katika familia Arecaceae. Matunda huitwa matende.

Asili ya miti hii ni ukanda kutoka Visiwa vya Kanari kupitia Afrika ya Kaskazini na Asia ya Kusini mpaka Malaysia na Uchina Kusini.

Mti unaojulikana sana ni mtende wa kawaida na mti huu hupandwa sana katika oasisi za majangwa ya Afrika na Asia na pembezoni kwa majangwa haya.

Mitende ni maarufu katika utamaduni wa Waisraeli na Waarabu. Injili ya Yohane 12:12-19 inataja matawi ya miti hiyo kwamba yalitumika kumshangilia Yesu alipoingia Yerusalemu kwa mara ya mwisho. Ndiyo sababu hadi leo matawi hayo yanatafutwa sana na Wakristo kwa maandamano ya Jumapili ya matawi, wiki moja kabla ya Pasaka.

Spishi nyingine humea katika vinamasi na misitu ya mikoko.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtende (mti) kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.