Jumapili ya matawi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Jumapili ya matawi ikiadhimishwa na Waorthodoksi wa Biškek huko Kirgizistan.
Mwaka wa liturujia
Magharibi
Mashariki

Katika mwaka wa Kanisa wa madhehebu mbalimbali ya Ukristo, Jumapili ya matawi ndiyo siku inapoadhimishwa jinsi Yesu Kristo alivyoingia Yerusalemu ili kufa na kufufuka kwa wokovu wa binadamu wote.

Siku hiyo alishangiliwa na umati kwa kutumia matawi, ndiyo asili ya jina.

Ndiyo mwanzo wa Juma kuu linaloadhimisha matukio makuu ya historia ya wokovu kadiri ya imani ya Wakristo.

Tangu mwaka 1985, kwa uamuzi wa Papa Yohane Paulo II, katika siku hiyo Kanisa Katoliki linaadhimisha pia "Siku ya kimataifa ya vijana", kwa sababu, kadiri ya Injili, watu wa rika hilo ndio waliomshangilia zaidi Yesu akiingia Yerusalemu.

ChristianitySymbol.PNG Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jumapili ya matawi kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.