Juma kuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Yesu kuingia Yerusalemu kwa shangwe kwenye Jumapili ya Matawi ndio mwanzo wa Juma kuu.
Mwaka wa liturujia
Magharibi
Mashariki

Juma kuu ni juma la mwaka ambalo Ukristo unaadhimisha kwa namna ya pekee matukio makuu ya historia ya wokovu kadiri ya imani yao, kuhusiana na mwisho wa maisha ya Yesu huko Yerusalemu, uliofuatwa na ufufuko wake.

Katika madhehebu mengi, juma hilo linaanza na Jumapili ya matawi ambapo linaadhimishwa kwa shangwe tukio la Yesu Kristo kuingia huo mji mtakatifu kama mfalme wa Wayahudi huku akipanda punda na kushangiliwa na umati wa wafuasi wake, waliofurahia hasa alivyomfufua Lazaro wa Betania.

Lakini Yesu alieleza kuwa ufalme wake si wa dunia hii, na kuwa yeye hakuja kutumikiwa bali kutumikia na kutoa uhai wake uwe fidia ya umati.

Hivyo siku zilizofuata alikabili kwa hiari mateso na kifo kutoka kwa wapinzani wake na kwa mamlaka ya Ponsio Pilato, na hatimaye akafufuka mtukufu usiku wa kuamkia Jumapili.

Kabla ya hapo Yesu alijumlisha hayo matukio yajayo katika karamu ya mwisho aliyokula pamoja na mitume wake 12, akiwaachia agizo la kufanya daima karamu ya namna hiyo kama ukumbusho wake.

Basi, kuanzia Alhamisi kuu jioni hadi Jumapili ya Pasaka jioni Wakristo wanaadhimisha siku tatu kuu za Pasaka, zinazofanya ukumbusho wa Yesu mteswa, mzikwa na mfufuka.

ChristianitySymbol.PNG Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Juma kuu kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.