Ijumaa Kuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Msalaba wa Ijumaa Kuu katika Catholicon kwenye Monasteri ya Utatu Mtakatifu, Meteora, Ugiriki.

Ijumaa Kuu ni siku ya mwaka ambayo wafuasi wengi wa Yesu Kristo wanaadhimisha kifo chake msalabani ambacho kilitokea nje ya kuta za mji wa Yerusalemu siku ya Ijumaa.

Kadiri ya Mtume Yohane kesho yake ilikuwa Sabato na pia Pasaka, jambo lisilotokea kwa kawaida. Kwa sababu hiyo wataalamu mbalimbali wanakadiria ilikuwa tarehe 7 Aprili 30.

Ijumaa kuu ni sehemu ya Juma Kuu linaloanza kwa adhimisho la Yesu kuingia mji huo akishangiliwa kama mfalme wa Wayahudi (yaani Masiya au Kristo). Adhimisho hilo linafanyika mwanzoni mwa wiki, yaani Jumapili ya matawi.

Ijumaa kuu ni pia sehemu ya siku tatu kuu za Pasaka zinazoadhimisha mateso na kifo chake, kulala kaburini, na hatimaye kufufuka kwa utukufu.

Waamini wakipokea ekaristi siku ya Ijumaa Kuu (Our Lady of Lourdes, Philadelphia, Marekani).
Njia ya Msalaba ikiadhimishwa kwenye Colosseum mjini Roma siku ya Ijumaa Kuu.
Picha ya El Greco ikimuonyesha Yesu akibeba msalaba, 1580.
Epitaphios ikionyesha mwili wa Yesu ukizikwa.
Epitaphios ikichukuliwa katika maandamano.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]