Pasaka ya Kikristo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Picha takatifu ya Ufufuko, ikimuonyesha Kristo akiwa amevunja milango ya kuzimu na kutoa Adamu na Eva nje ya makaburi. Kristo anazungukwa na watakatifu, huko Shetani, aliyechorwa kama mzee, amefungwa kwa minyororo.
Mwaka wa liturujia
Magharibi
Mashariki
Tarehe za Pasaka kwa miaka 2000-2020
Mwaka Ukristo wa Magharibi
(Kalenda ya Gregori)
Ukristo wa Mashariki
(Kalenda ya Juliasi)
2000 23 Aprili 30 Aprili
2001 15 Aprili
2002 31 Machi 5 Mei
2003 20 Aprili 27 Aprili
2004 11 Aprili
2005 27 Machi 1 Mei
2006 16 Aprili 23 Aprili
2007 8 Aprili
2008 23 Machi 27 Aprili
2009 12 Aprili 19 Aprili
2010 4 Aprili
2011 24 Aprili
2012 8 Aprili 15 Aprili
2013 31 Machi 5 Mei
2014 20 Aprili
2015 5 Aprili 12 Aprili
2016 27 Machi 1 Mei
2017 16 Aprili
2018 1 Aprili 8 Aprili
2019 21 Aprili 28 Aprili
2020 12 Aprili 19 Aprili

Pasaka ya Kikristo ni sikukuu ya kufanya ukumbusho wa kufufuka kwake Yesu Kristo siku ya tatu baada ya kusulubiwa, kufa na kuzikwa kwake.

Inahesabiwa kuwa sikukuu muhimu kabisa katika madhehebu mengi ya Ukristo, kwa sababu ufufuko huo ndio msingi wa imani ya Kikristo. Mtume Paulo aliandika kwamba Kristo asingefufuka, imani hiyo ingekuwa haina maana, kwa kuwa asingeondolea dhambi za watu.

Jina la Pasaka[hariri | hariri chanzo]

Jina la "Pasaka" limetokana na sherehe ya Pasaka ya Kiyahudi linaloitwa "פסח" (tamka: pasakh) kwa lugha ya Kiebrania. Kwa Kiswahili majina ya sherehe za Kikristo na Kiyahudi hazitofautiani.

Asili yake ni kwamba kusulibiwa na kufufuka kwa Yesu Kristo kumetokea wakati wa sikukuu ya Pasaka ya Kiyahudi mnamo Aprili ya mwaka 30 BK.

Wakristo wa kwanza, ambao wote walikuwa Wayahudi, walisheherekea sikukuu ya Kiyahudi pamoja na kumbukumbu ya ufufuko wa Yesu. Baadaye sherehe na pia tarehe zikawa tofauti.

Tarehe ya Pasaka[hariri | hariri chanzo]

Tarehe ya Pasaka inafuata kuonekana kwa mwezi angani, kwa hiyo sikukuu hiyo haina tarehe imara katika kalenda ya kawaida. Inapatikana katika Machi au Aprili. Pasaka haifuati mwezi pekee lakini tarehe yake imefungwa pia kwa sikusare (au ekwinoksi), kwa hiyo haiendelei kuzunguka mwaka wote kama tarehe za Kalenda ya Kiislamu.

Mtaguso wa kwanza wa Nisea mwaka 325 uliamua ya kwamba Pasaka itasheherekewa Jumapili ya kwanza baada ya mwezi mpevu wa kwanza baada ya 21 Machi (tarehe ya sikusare machipuo ambayo ni siku ya usawa wa mchana na usiku, hivyo mwanzo wa majira ya kuchipua kaskazini mwa dunia). Kwa kuwa mwezi mpevu baada ya 21 Machi inaweza kutokea kati ya 22 Machi na 19 Aprili, tarehe ya Pasaka, ambayo ni Jumapili inayofuata, hutokea kati ya 22 Machi na 25 Aprili.

Katika Ukristo kuna kalenda mbili zinazotumika, hivyo pia tarehe mbili za Pasaka. Kanisa la magharibi, yaani Wakatoliki wengi na Waprotestanti, hufuata Kalenda ya Gregori (ambayo imekuwa kalenda ya kawaida ya kimataifa), lakini Waorthodoksi wanaendelea kutumia kalenda iliyotangulia, yaani Kalenda ya Juliasi. Ndiyo maana mara nyingi Pasaka inaendelea kuadhimishwa katika Jumapili tofauti kati ya pande hizo mbili. Hata hivyo kuna majadiliano yenye lengo la kufikia makubaliano ili kuadhimisha Pasaka pamoja.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Liturujia
Mapokeo
Hesabu
ChristianitySymbol.PNG Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pasaka ya Kikristo kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.