Njia ya Msalaba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kituo cha 10 – Yesu akivuliwa. Kanisa kuu la Santiago de Compostela, Hispania.
Kituo cha 12 – Yesu akifa msalabani. St. Raphael's Cathedral, Dubuque, Iowa, Marekani.
Njia ya msalaba ilivyopangwa katika kanisa kuu la Hong Kong, China.
Station 5: Simoni wa Kirene akimsaidia Yesu kubeba msalaba, Maandamano ya Ijumaa Kuu 2011 huko Ulm, Ujerumani.


Njia ya Msalaba (kwa Kilatini, Via Crucis au Via Dolorosa) ni desturi ya sala inayolenga kumfuata Yesu Kristo hadi msalabani na kaburini.

Desturi hiyo ilianza Wakristo wa Ulaya walipozidi kutembelea Nchi takatifu katika Karne za Kati. Ni hasa wafuasi wa Fransisko wa Asizi walioeneza desturi hiyo kila mahali.[1]

Mengi kati ya makanisa ya Wakatoliki yaani picha 14 zilizopangwa kwa kawaida ukutani kwa umbali fulani ili kuwezesha waamini kutembea kati ya moja na nyingine huku wakiendelea kutafakari juu ya mateso ya Yesu, jinsi ambavyo wangefanya mjini Yerusalemu, ili kuelewa zaidi upendo wa Mungu, kuchukia dhambi na kuzifidia.[2][3]

Hata baadhi ya Walutheri na Waanglikana wanapenda desturi hiyo.[4][5]

Desturi hiyo inaweza kufuatwa na mtu mmojammoja au kwa makundi hata makubwa.[6]

Mbali ya kila Ijumaa ya mwaka, waamini wengi wanafuata njia hiyo wakati wa Kwaresima, na kwa namna ya pekee Ijumaa Kuu.[7]

Mbali ya vituo 14 vilivyozoeleka zaidi, wengine wanapenda kuviongeza, kuvipunguza au kuvibadilisha hasa kwa kufuata zaidi habari za Injili[8][9] na kumalizia na ufufuko wake.[10][11]

Gallery[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

 1. Schiller, Gertrud, Iconography of Christian Art, Vol. II, p. 82, 1972 (English trans from German), Lund Humphries, London, ISBN 0-85331-324-5
 2. Miserentissimus Redemptor, Encyclical of Pope Pius XI
 3. Pope John Paul II, Letter to Cardinal Fiorenzo Angelini, for the 50th anniversary of the Benedictine Sisters of Reparation of the Holy Face, 27 September 2000 (Vatican archives)
 4. "Trinity Evangelical Lutheran Church". Trinitycamphill.org. 2014-04-08. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-02-22. Iliwekwa mnamo 2014-07-03. 
 5. Pastor Zip (2007-04-06). "Pastor Zip's Blog: The Stations of the Cross". Pastorzip.blogspot.com. Iliwekwa mnamo 2014-07-03. 
 6. "CATHOLIC ENCYCLOPEDIA: Way of the Cross". Newadvent.org. 1912-10-01. Iliwekwa mnamo 2014-07-03. 
 7. Ann Ball, 2003 Encyclopedia of Catholic Devotions and Practices ISBN 087973910X
 8. Joseph M Champlin, The Stations of the Cross With Pope John Paul II Liguori Publications, 1994, ISBN 0-89243-679-4
 9. Pope John Paul II, Meditation and Prayers for the Stations of the Cross at the Colosseum Archived 3 Juni 2013 at the Wayback Machine., Good Friday, 2000
 10. "The Official Web Site for the Archdiocese of Detroit". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-12-23. Iliwekwa mnamo 2012-02-13. In some contemporary Stations of the Cross, a fifteenth station has been added to commemorate the Resurrection of the Lord. 
 11. "Fr. William Saunders". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-04-30. Iliwekwa mnamo 2009-04-04. Because of the intrinsic relationship between the passion and death of our Lord with His resurrection, several of the devotional booklets now include a 15th station, which commemorates the Resurrection. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Njia ya Msalaba kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.