Kigamboni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kata ya Kigamboni
Kata ya Kigamboni is located in Tanzania
Kata ya Kigamboni
Kata ya Kigamboni
Mahali pa Kigamboni katika Tanzania
Viwianishi: 6°52′8″S 39°15′40″E / 6.86889°S 39.26111°E / -6.86889; 39.26111
Nchi Tanzania
Mkoa Dar es Salaam
Wilaya Temeke
Idadi ya wakazi
 - 30,496
Feri ya Kigamboni mjini Daressalaam
Mapumziko Kigamboni ufukoni


Kigamboni ni jina la Wilaya katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania yenye postikodi namba 17000[1] . Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ina wakazi wapatao 30,496 waishio humo.[2]

Kigamboni ina umbo la rasi kati ya Bahari Hindi na maji ya bandari. Imetengwa na jiji la Dar es Salaam kwa maji ya Kurasini Creek.

Mawasiliano yapo kwa njia ya feri kati ya Kigamboni na Kivukoni upande wa jiji. Kuna pia barabara inayozunguka bandari lakini njia hii ni ndefu mno ni kilomita zaidi ya hamsini hadi kitovu cha jiji kwa njia ya nchi kavu. Kuna mipango ya kujenga daraja.

Pia Kigamboni katika kata ya Vijibweni ndiyo sehemu ambapo kuna yadi nyingi za mafuta k.mf. kampuni zinazohifadhi mafuta katika yadi hizo ni: CAMEL OIL, OIL COM, BIG BON na nyinginezo.

Kiasili sehemu hii ilikuwa kijiji cha wavuvi lakini katika miaka ya nyuma watu wa jijini wamejenga nyumba na hoteli za kitalii zimeenea kwenye ufuko wa Bahari Hindi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Temeke - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Azimio | Buza | Chamazi | Chango'mbe | Charambe | Keko | Kibada | Kiburugwa | Kigamboni | Kijichi | Kilakala (Temeke) | Kimbiji | Kisarawe II | Kurasini | Makangarawe | Mbagala | Mbagala Kuu | Mianzini | Miburani | Mji Mwema | Mtoni | Pemba Mnazi | Samangira | Sandali | Tandika | Temeke (kata) | Toangoma | Tungi | Vijibweni | Yombo Vituka