Kigamboni (kata)
Kigamboni ni kata ya wilaya ya Kigamboni iliyo na postikodi namba 17107.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 24,810 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 30,496 waishio humo.[2]
Kigamboni ina umbo la rasi kati ya Bahari Hindi na maji ya bandari. Imetengwa na jiji la Dar es Salaam kwa maji ya Kurasini Creek.
Mawasiliano yapo kwa njia ya feri kati ya Kigamboni na Kivukoni upande wa jiji.
Kiasili sehemu hii ilikuwa kijiji cha wavuvi lakini katika miaka ya nyuma watu wa jijini wamejenga nyumba na hoteli za kitalii zimeenea kwenye ufuko wa Bahari Hindi.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ http://www.meac.go.tz/sites/default/files/Statistics/Tanzania%20Population%20Census%202012.pdf Ilihifadhiwa 2 Januari 2004 kwenye Wayback Machine. Wilaya ya Temeke - Mkoa wa Dar es Salaam
Kata za Wilaya ya Kigamboni - Tanzania | ||
---|---|---|
Kibada (17109) | Kigamboni (17107) | Kimbiji (17101) | Kisarawe II (17104) | Mjimwema (17106) | Pembamnazi (17105) | Somangila (17102) | Tungi (17103) | Vijibweni (17108) |
Makala hii kuhusu maeneo ya Dar es Salaam bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kigamboni (kata) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |