Kibada (Dar es Salaam)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Kata ya Kibada
Kata ya Kibada is located in Tanzania
Kata ya Kibada
Kata ya Kibada

Mahali pa Kibada katika Tanzania

Majiranukta: 6°52′8″S 39°15′40″E / 6.86889°S 39.26111°E / -6.86889; 39.26111
Nchi Tanzania
Mkoa Dar es Salaam
Wilaya Kigamboni
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 3,305

Kibada ni kata mojawapo ya Wilaya ya Kigamboni katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ina wakazi wapatao 3,305 waishio humo.[1]

Kibada ina jumla ya mitaa sita ambayo ni Kiziza, Nyakwale, Kifurukwe, Uvumba, Sokoni na Kichangani.

Upimaji wa viwanja kwa ajili ya makazi, ulihusisha mitaa miwili tu, yaani mtaa wa Kichangani na mtaa wa Kifurukwe.

Zahanati ipo eneo la stendi ya Kibada iliyo karibu na njia panda ya Dar es Salaam Zoo, Kisiwani, Kongowe na Mjimwema.

Jirani na zahanati, kuna kituo cha polisi, nyuma yake kuna jengo la kigango cha Kanisa Katoliki.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 2002 Population and Housing Census General Report (en). Government of Tanzania. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-02-10. Iliwekwa mnamo 2008-08-21.
Kata za Wilaya ya Kigamboni - Tanzania

Kibada (17109) | Kigamboni (17107) | Kimbiji (17101) | Kisarawe II (17104) | Mjimwema (17106) | Pembamnazi (17105) | Somangila (17102) | Tungi (17103) | Vijibweni (17108)