Ubungo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtazamo wa angani wa Wilaya ya Ubungo unaoangalia kampuni ya umeme ya TANESCO kushoto.

(makala hii inahusu kata ya Ubungo, kuangalia makala ya Wilaya ya Ubungo bonyeza hapa)


Kata ya Ubungo
Kata ya Ubungo is located in Tanzania
Kata ya Ubungo
Kata ya Ubungo

Mahali pa Ubungo katika Tanzania

Majiranukta: 6°47′42″S 39°15′58″E / 6.79500°S 39.26611°E / -6.79500; 39.26611
Nchi Tanzania
Mkoa Dar es Salaam
Wilaya Ubungo

Ubungo ni jina la kata ya wilaya ya Ubungo katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania yenye postikodi namba 16103[1].

Ubungo ipo katika sehemu ya kati ya magharibi mwa wilaya na inafahamika sana Tanzania kama kitovu kikuu cha Mabasi yaelekeayo mikoani.

Kituo cha mabasi cha Ubungo kimeungana na baadhi ya vituo vikubwa vya miji mbalimbali ya Tanzania kama vile cha Arusha, Moshi, Morogoro, Dodoma, Mbeya, Iringa, Mtwara, Lindi, Singida, Tanga na Mwanza; vilevile hadi Nairobi, Lilongwe, Lusaka na miji mingine kadhaa ya Afrika ya Mashariki.

Pia Ubungo ndipo palipo makao makuu ya TANESCO, shirika la umeme la Tanzania.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Ubungo - Mkoa wa Dar es Salaam - Tanzania

Goba | Kibamba | Kimara (Ubungo) | Kwembe | Mabibo | Makuburi | Makurumla | Manzese | Mbezi | Mburahati | Msigani | Saranga | Sinza | Ubungo