Sanamu ya Askari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Sanamu ya askari, Dar es Salaam.
Historia ya Tanzania
Coat of Arms of Tanzania
This article is part of a series
Uendo
Historia ya Zanzibar
Ukoloni
Mgawanyo wa Afrika
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Mkataba wa Zanzibar-Helgoland
Mkwawa
Vita vya Maji Maji
Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki
Tanganyika
Uhuru
Mapinduzi ya Zanzibar
Julius Nyerere
Ujamaa
Tamko la Arusha
Vita vya Kagera
Ali Hassan Mwinyi
Benjamin Mkapa
Jakaya Kikwete
{Kigezo:Data99

Tanzania Portal

Sanamu ya Askari au Askari Monument ni sanamu iliyopo penye kitovu cha jiji la Dar es Salaam mahali ambapo mitaa ya Samora na Azikiwe (zamani: Maktaba) zinakutana.

Sanamu inamwonyesha askari Mwafrika katika sare ya kijeshi ya King's African Rifles wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia (1914-1918) akishika bunduki yenye kisu cha kando na kutazama upande wa bahari.

Iliwekwa na Waingereza mwaka 1927 kama kumbukumbu ya askari na wapagazi Waafrika waliopiga vita hivyo katika Afrika ya Mashariki hasa kati ya Uingereza na Ujerumani ambao wengi wao walikufa.

Kuna maandishi ya kumbukumbu kwa Kiingereza na Kiswahili kilichoandikwa kwa herufi za Kiarabu na herufi za Kilatini pia.

Maneno yake kwa Kiswahili ni kama yafuatayo:

"Huu ni ukumbusho wa askari Waafrika wenyeji waliopigana katika Vita Kuu na ni ukumbusho pia kwa wapagazi ambao walikuwa miguu na mikono ya majeshi. Ni ukumbusho pia kwa watu wote waliotumika wakafa kwa ajili ya mfalme na nchi yao katika Afrika ya Mashariki kwenye Vita Kuu toka mwaka 1914 mpaka 1918 . Ukipigania nchi yako ujapo umekufa watoto wako watalikumbuka jina lako."

Mahali pa sanamu hii iliwahi kuwa na sanamu ya meja Hermann von Wissmann aliyekuwa gavana wa kwanza wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na sanamu hiyo ilibomolewa na Waingereza walipoteka mji katika mwaka 1916.

Picha[hariri | hariri chanzo]