Wilaya ya Kinondoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya angani ya Wilaya ya Kinondoni mnamo mwaka 2015.
Mahali pa Kinondoni (kijani) katika mkoa wa Dar es Salaam.

Wilaya ya Kinondoni ni moja ya wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam yenye postikodi namba 14000[1] . Kwa lugha nyingine ni manisipaa ndani ya jiji la Dar Es Salaam. Eneo lake ni sehemu za kaskazini za jiji. Kinondoni inaanza upande wa pwani kwenye Selander bridge juu ya mto Upanga (pia: Msimbazi Creek) na kuendelea kupitia rasi ya Msasani, Kunduchi hadi Mbweni pamoja na hoteli za kitalii zilizopo sehemu hizi.

Barani inaelekea kuvukia barabara ya Morogoro hadi Mbezi na Kibamba. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kipo ndani ya manisipaa hii.

Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa Kinondoni ilihesabiwa kuwa 1,775,049 [2].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Kinondoni - Tanzania

BunjuHananasifKaweKigogoKijitonyamaKinondoniKunduchiMabwepandeMagomeni (Dar es Salaam)MakongoMakumbushoMbezi juuMbweniMikocheniMsasaniMwananyamalaMzimuniNdugumbiTandaleWazo