Nenda kwa yaliyomo

Mabwepande

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Kata ya Mabwepande
Nchi Tanzania
Mkoa Dar es Salaam
Wilaya Kinondoni
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 66,794

Mabwepande ni kata ya Wilaya ya Kinondoni katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania, yenye postikodi namba 14134.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 66,794 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 25,460 waishio humo. [2].

Mabwepande ina msitu mkubwa ambao unaitwa msitu wa Pande. Msitu huu unajulikana kwa vitendo vya kigaidi ambapo Dr. Ulimboka alifanyiwa vitendo vya kigaidi katika msitu huo.

Ndani ya Mwabepande kuna mji mpya uitwao Kinondo unaokuja kwa kasi, ila wakazi wake wanalalamikia kutokuwa na daraja.

Kipindi cha mvua, Kinondo inageuka kuwa kisiwa, hivyo watoto wanashindwa kuenda shule. Pia mitaa mingine ambayo inapatikana Mabwepande ni Manzese, Banana, Monduli, Malolo, Mji mpya, Vikawe na Njechele.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewahi kufika katika kata hiyo kutatua migogoro ya ardhi.[3]

Historia ya Mabwepande

[hariri | hariri chanzo]

Inasadikika kuwa hapo zamani Mabwepande ilikuwa ikiiitwa Mawepande kwa sababu kulikuwa na mawe makubwa mawili na msitu wa Pande, lakini ujio wa Wazungu ulibadilisha jina hilo kwa sababu walikuwa hawawezi kulitamka vizuri na kupelekea kuitwa Mabwepande.

  1. https://www.nbs.go.tz/
  2. "Ripoti Kuu ya Sensa ya Watu na Makazi kwa Mwaka wa 2012" (kwa Kiingereza). Serikali ya Tanzania. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-05-11. Iliwekwa mnamo 15-12-2013. {{cite web}}: Check date values in: |accessdate= (help)
  3. https://www.facebook.com/247412001951938/photos/wananchi-wanaodaiwa-kuvamia-shamba-la-waziri-mkuu-mstaafu-fredrick-sumaye-lililo/1262424543784007/
Kata za Wilaya ya Kinondoni - Tanzania

BunjuHananasifKaweKigogoKijitonyamaKinondoniKunduchiMabwepandeMagomeniMakongoMakumbushoMbezi JuuMbweniMikocheniMsasaniMwananyamalaMzimuniNdugumbiTandaleWazo