Wilaya ya Wanging'ombe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wilaya ya Wanging'ombe ni wilaya moja ya Mkoa wa Njombe. Ilianzishwa mwezi wa Machi 2012. Kabla ya hapo ilikuwa sehemu ya magharibi ya Wilaya ya Njombe katika Mkoa wa Iringa. Tangu Njombe kuwa mkoa wilaya ya Njombe ya awali iligawiwa kwa wilaya za Wanging'ombe, Njombe Mjini na Njombe Vijijini.

Makao makuu ni kata ya Igwachanya. Wakati wa sensa ya mwaka 2012 wilaya hii ilikuwa na wakazi 161,816.[1].

Kata[hariri | hariri chanzo]

Wilaya ya Wanging'ombe ilipoanzishwa, ikawa na kata 16:

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya 2012, Njombe Region
Kata za Wilaya ya Wanging'ombe - Tanzania

Igima | Igosi | Igwachanya | Ilembula | Imalinyi | Kidugala | Kijombe | Kipengele | Luduga | Makoga | Mdandu | Saja | Uhambule | Ulembwe | Usuka | Wangama | Wanging'ombe