Ilembula

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kata ya Ilembula
Nchi Tanzania
Mkoa Njombe
Wilaya Wanging'ombe
Idadi ya wakazi
 - 18,174

Ilembula ni jina la kata ya Wilaya ya Wanging'ombe katika Mkoa wa Njombe, Tanzania. Wakati wa wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 15,642 [1] walioishi humo. Msimbo wa posta ni 59305

Ndani ya kata kuna vijiji vya Ilembula Kati, Iponda, Igelehedza na Igula. Wenyeji walio wengi ni Wabena wanaolima hasa mahindi na maharagwe. Vinywaji vinavyopendwa ni ulanzi, pombe na togwa.

Ilembula Kati, Igelehedza na Igula kuna shule ya msingi. Taasisi kubwa ni hospitali ya kiluteri na chuo chake.

Dini[hariri | hariri chanzo]

Ilembula imekuwa kitovu cha kazi ya Walutheri katika Ubena tangu 1906 mwaka wamisonari Wajerumani walipofika. Leo hii Ilembula Kati ni makao makuu ya Jimbo la Kilutheri ndani ya Dayosisi ya Kusini KKKT. Kanisa hili linaendesha hospitali ya kilutheri yenye vitanda 240 pamoja na chuo cha wauguzi chenye wanafunzi 143.www.ilembulanursing.ac.tz

Kanisa katoliki lina kitovu chake kwenye kijiji cha Igelehedza pamoja na shule ya vidudu na shule ya maarifa ya nyumbani. Madhehebu mengine kama vile Assemblies of God, Wapentekoste, Wasabato na Mashahidi wa Yehova wako pia hata kama si wengi. Nao Waislamu wako wana misikiti katika Igelehedza.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya 2012, Njombe - Wanging'ombe DC
Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Wanging'ombe - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Igima | Igosi | Igwachanya | Ilembula | Imalinyi | Kidugala | Kijombe | Kipengele | Luduga | Makoga | Mdandu | Saja | Uhambule | Ulembwe | Usuka | Wangama | Wanging'ombe


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Njombe bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ilembula kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.