Nenda kwa yaliyomo

Togwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Togwa ni kinywaji baridi kinachotengenezwa kwa nafaka au maji ya matunda. Namna ya kutengeneza ni sawa na pombe ya kawaida ila tu haikubadilika bado kuwa na alikoholi.

Togwa ndiyo itakuwa pombe ikikaa. Kwa mfano, togwa ya ulanzi ni utomvu kutoka mianzi baada ya masaa kadhaa, na ulanzi wenye pombe ni utomvu uleule kutoka mianzi baada ya siku mbili hivi.

Nafaka zinazotumika kutengenezea zaidi huwa ni mtama au mahindi.

Jinsi ya kutengeneza togwa la mtama

Kwanza chukua mtama mkavu uoshe na uuweke kwenye chombo kikavu alafu uufunike kwa muda wa siku 2,ukifunua utakuta umeanza kuota(kimea) chukua mtama mwingine uloweke kwa siku moja alafu uusage,unga wake pika uji wa saizi ya kati si mzito si mwepesi.Uache ule uji upowe,ukisha poa chukua kile kimea(mtama ulioanza kuota) usage kidogo ili kubakia na chenga chenga.Alafu mimina zile chenga chenga za kimea kwenye ule uji.Tia sukari unaweza kunywa baada ya nusu saa na kuendelea.


Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Togwa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.