Majadiliano:Togwa

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Togwa - pombe??[hariri chanzo]

Je kuna tofauti gani kati ya togwa na pombe la kawaida? Yaani pombe ya mahindi, ulezi na kadhalika? Ni aina tofauti au aina ya pekee au ni lugha ya eneo tu? --Kipala 16:45, 25 Agosti 2007 (UTC)[jibu]

Nadhani ni tofauti za kimaeneo. Lakini ngoja niulize watu wengine. Ndesanjo, 25 Agosti 2007

Kumbe kamusi ya KKK/SED yasema: "togwa , native beer (pombe) in the sweet, unintoxicating state, not fermented". Kumbe ni kama divai changa kwenye nchi za Mediteranea ambayo ni zaidi kama maji ya mizabibu. --Kipala 22:56, 25 Agosti 2007 (UTC)[jibu]

Lakini katika Kamusi ya kiswahili sanifu yasema: Togwa ni kinywaji kisicholeyva kinachotengenezwa kwa kimea, unga wa mtama au ulezi na sukari. --Joel Niganile 16:47, 26 Agosti 2007 (UTC)[jibu]

BAsi naona ni ileile hakuna tofauti. Sijui togwa lakini kutokana na maelezo yako nadhani ya kwamba togwa itabadilika kuwa pombe isiponyewa yaani ikiachwa vile itaanza kuchachuka. Kweli? Au kuna mbinu inayozuia kuchachuka na kuwa na kiwango cha pombe ndani yake? --Kipala 17:20, 26 Agosti 2007 (UTC)[jibu]

Nimepeleka swali huko Kamusi_Hai inaonekana togwa ni hali ya pombe kabla haijachachuka na kujenga alikoholi. (http://research.yale.edu/swahili/learn/en/node/566#comment-1517).

Swali kwa Joel: Je una uhakika ya kwamba togwa ya mtama haikuchachuka bado baada ya siku mbili? Yaani kuwa pombe tayari?? --Kipala 07:47, 27 Agosti 2007 (UTC)[jibu]